Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Siku moja baada ya walemavu kupata usaidizi mbalimbali kutoka kwa mbunge wa Saku Dido Ali Raso na Senata wa Marsabit Mohamed Chute, watu wanaoishi na ulemavu wa kutozungumza wamekariri kuwa wanapitia changamoto nyingi katika kaunti hii.
Baadhi ya waliozungumza na Idha hii wamesema kuwa changamoto kuu wanayokumbana nayo na kukosekana kwa watasfri jambo linalolemaza mazungumzo na maelewanao kati yaoa na watu wengine haswa wanaposaka hudumu mbalimbali katika jamii.
Hata hivyo wametoa wito wa kuwepo angalao kwa mfasiri kwenye hafla zinazoandaliwa hapa jimboni.
Wengine wao wamelalamikia ukosefu wa njia maalum wanayofaa kutumia haswa wanaotumia magari ya magurumu maarufu (wheel chairs) wanapotembelea afisi za serekali huku wakitaka hilo kuangaziwa.
Aidha baadhi ya watu wanaoishi na ulemavu wamelalamikia kile wamekitaja kuwa ni kutengwa katika mgao wa pesa za mradi wa inua jamii unaolenga watu wanaoishi na ulemavu pamoja na makundi mengine huku wakiirai serekali kuhakikisha kwamba wanapata fedha hizo bila kubaguliwa.