WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Wanaume wawili wa umri wa makamu wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kosa la wizi wa kimabavu.
Mahakama ya Marsabit imeelezewa kuwa mnamo tarehe 21 mwezi Agosti mwaka 2023 katika makutano ya Muslim Agency, Marsabit mjini Kuri Roba Sora na Halkano Guyo Halakhe kwa ushirikiano na mshukiwa mwingine moja wakiwa wamejihami kwa bunduki aina ya Pistol walimvamia mhudumu moja wa bodaboda, wakaiba bodaboda na kisha kumdhulumu mhudumu huyo.
Wawili hao walikamatwa tarehe 22 mwezi huo wa Agosti na kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tarehe 28 mwezi uo huo.
Akitoa hukumu dhidi ya wawili hao hii leo hakimu mkuu mwandamizi Christine Wekesa amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa visa hivyo wawili hao watakuwa mfano kwa watu wanaotekeleza visa kama hivyo.
Wawili hao wana siku 14 kukata rufaa.