Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na JB Nateleng,
Naibu gavana wa Marsabit Solom Gubo amewataka wakazi wa Marsabit kuweza kujipanga vyema kabla ya msimu wa mvua fupi za mwezi Oktoba/Novemba.
Akizungumza na idhaa hii baada ya mkutano wa kamati ya maalum ya kushughulikia majanga katika jimbo la Marsabit CSG hii leo Gubo amesema kuwa idara ya utabiri ya hali ya hewa jimboni imearifu kuwa, kaunti ya Marsabit itapokea mvua ya kiwango cha wastani msimu huu na kuwataka wanachi kujiandaa ipasavyo.
Gubo amezitaka idara tofauti ya serekali kuweza kuwajibika katika kupeana taarifa zinazofaa kwa wakazi jimboni ili kuwaelimisha kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa jimboni.
Aidha Gubo amesema kuwa serekali ya kaunti pamoja na washikadau tofauti watashirikiana ili kutafta mbinu mbadala iwapo mvua itakawia kunyesha jimboni.
Kuhusiana na swala la ukeketaji, Gubo amwataka viongozi wote kukemea vitendo na kusaidia katika kupinga visa vya ukeketaji pamoja na ndoa za mapema jimboni ambavyo vinaadhiri watoto wa kike.