HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Caroline Waforo,
Wakaazi jimboni Marsabit wamehimizwa kujisajili kwa bima mpya ya SHIF.
Ni wito ambao umetolewa na naibu kamishna wa Marsabit ya kati David Saruni ambaye amezungumza na Shajara Ya Radio Jangwani.
Kulingana na Saruni bima hii mpya ya afya itawawezesha wananchi wote kupata matibabu ya bure.
Saruni amewataka wakaazi kutupilia mbali dhana kuwa hawatanufaika pakubwa na bima hii ya SHIF ikilinganishwa na bima za kibinafsi.
Kadhalika amewaeleza wakaazi jimboni taratibu za kufuata iili kujisajili kwa bima hii mpya.
Bima hiyo itakayoanza kutekelezwa Oktoba 1 mwaka huu itachukua mahali pa Bima ya Afya ya Kitaifa ya NHIF.