KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
NA GRACE GUMATO
Wakaazi wa Forolle na Elebor wamehimizwa kuishi kwa amani wakati ambao usalama unazidi kuimarishwa katika mipaka ya Kenya na Ethiopia.
Akizungumza katika mkutano wa usalama unaofanyika katika maeneo yanayopakana na nchi jirani ya Ethiopia kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amewahakikishia wakaazi hao usalama wa kutosha kwa kuahidi kuajiri askari wa akiba NPR katika eneo hilo na kuwahimiza wakaazi kushirikiana na asasi za usalama ili hali ya utulivu iweze kurejea katika eneo hilo.
Wakti uo huo wakaazi wa eneo la Forolle wameomba usalama kuimarishwa katika barabara za eneo hilo wakisema kuwa shughuli za kibiashara zimetatizika mno.
Waakazi hao pia wameiomba serikali kuifanya Forolle kuwa katika kaunti ndogo akitaja kuwa kwa sasa wako katika kaunti ndogo ya Maikona na kupata huduma za serikali imekuwa ngumu sana na pia wakiomba serikali kuimarisha usalama ili watoto warejee shuleni.