IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
Na JB Nateleng
Wito umetolewa kwa idara ya kilimo pamoja na serekali ya kaunti ya Marsabit kuweza kuwasaidia wakulima katika utayarishaji wa mashamba wanaposubria msimu wa mvua.
Wakizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, mzee Wako Gusia ambaye ni mzee wa manyatta Konso Dakabaricha, eneobunge la Saku kaunti ya Marsabit amesema kuwa itakuwa ni afueni kwa wakulima katika eneo la Saku iwapo serekali itaingilia kati na kuwasaidia katika maandalizi ya mashamba yao kwani kuna wengi ambao hawana uwezo wa kuweza kutayarisha shamba vyema na kuweza kupata mavuno mengi.
Mzee Wako amesema kuwa hangetaka wakulima kukadiria hasara kama ilivyokuwa msimu uliopita kwa sababu ya kutojipanga mapema.
Hata hivyo Mzee Wako amewachangamoto wakulima wenza ambao walikuwa wamekakufa moyo na kuacha mashamba yao bila kulima baada ya kupata hasara kuweza kurejea katika upanzi na utayarishaji wa mashamba kwa ajili ya msimu ujao wa mvua.
Wakati huo huo mzee Mohamed Tarikokumsa, kutoka manyatta ya Konso Dakabaricha eneo la Saku ameirai serekali pia kuweza kuingilia kati katika kuhakikisha kuwa wakulima wamepata mbegu kwa wakati, pembejeo kwa urahisi na pia kuwafunza kilimo bora ambayo itawasaidia kupata mavuno mengi.