WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Polisi mjini Marsabit wanamzuilia mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 37 ambaye aliyekamatwa jana jioni kwa makosa ya wizi katika duka la MPesa mjini Marsabit.
Akidhibitisha kisa hicho OCS wa Marsabit Central Edward Mabonga ametaja kwamba mhalifu kwa jina Musei Ndemwa alitiwa mbaroni jana jioni katika eneo la Frontline karibu na Saku Bar katika shughuli ya wizi wa pesa kupitia simu ya rununu.
Anasema kuwa mshukiwa alifika katika duka hilo mida ya saa moja unusu jioni kwa lengo la kutoa pesa ila akajifanya kwamba anaongea na mtu aliyejifanya kuwa muhudumu wa kampuni ya Safaricom ambapo walimpa maagizo mwenye duka la Mpesa na kisha kumpora kitita cha shilingi elfu 69.
Aidha Mabonga ameweka wazi kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini anaoshirikiana nao na hata mbinu wanyoitumia kuwakoni watu fedha zao.