Mwanaume moja wa miaka 38 ameponea kifo baada ya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga kutibuka usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha Soweto mjini Laisamis kaunti ya Marsabit.
February 7, 2025
Na JB Nateleng & Naima Abdullahi,
Mwanamme mmoja aliyeripotiwa kupotea miezi mitatu iliyopita amepatikana akiwa ameiga dunia katika crater ya Goff Arero eneo bunge la Saku,kaunti ya Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee chifu wa eneo Qiltu Korma Alex Ali Goresa, amesema kuwa mwanamme huyo na ambaye alikuwa na matatizo ya akili amezikwa hii leo katika eneo la Manyatta Athi Huka.
Chifu Gores ahata hivyo ametoa wito kwa wakazi jimboni Marsabit kuwachunga na kuwashughulikia watu wanaoishi na matatizo ya kiakili ili kuweza kudhibiti visa kama hivi kutokea siku za usoni.