Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Serikali ya kaunti ya Marsabit,idara ya utawala na huduma za umma kwa ushirikiano na mashirika yasiyo ya kiserikali ya HODI chini ya ufadhili wa global giving imeweka mipangilio ya kutenga fedha za kushughulikia majanga katika kaunti ya Marsabit maarufu (DRM).
Kwa mujibu wa waziri wa utawala katika serekali ya kaunti ya Marsabit Dkt. Armara Galwab ni kuwa mpangilio huo utawezesha kaunti ya Marsabit kushughulikia majanga iwapo yatajiri.
Akizungumza wakati wa kupokea ripoti kuhusiana na mipangilio hiyo waziri Galwab amekariri kuwa kamati maalum pia imebuniwa ili kurahisisha kushughulikia majanga hapa jimboni.
Aidha Galwab amesema kuwa idara mbalimbali katika kaunti ya Marsabit zitakuwa na nafasi ya kutoa angalau asilimia moja ya fedha za bajeti yao ambazo zitaelekezwa katika mgao huo.
Hata hivyo Galwab amesema kuwa serekali ya kaunti ya Marsabit imekamilisha mikakati yote hitajika ili kuhakikisha kwamba mgao huo wa kushughulikia majanga (DRM) unatekeleza majuku yake ipasavyo kuanzia mwaka ujao wa 2025.