HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na JB Nateleng,
Mashindano ya watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti ya Marsabit yazinduliwa rasmi hii leo.
Akizungumza baada ya mashindano hayo waziri wa jinsia katika kaunti ya Marsabit Jeremy Ledanyi amesema kuwa idara ya jinsia Jimboni itaendelea kuhamasisha jamii kuhusiana na watu wanaoishi na ulemavu,kutambua talanta zao na kubuni mbinu mbadala ambazo zitawasaidia kuboresha na kuinua talanta hizo.
Ledanyi ameelezea kuwa idara hiyo itashirikiana na washikadau tofauti kuhakikisha kuwa mashindano haya yameandaliwa kila mwaka ili kuwatambua na kuwainua walemavu.Waziri Ledanyi amesema kuwa mashindano haya pia yanadhamiria kuleta usawa katika jamii.
Wakati uo huo, Naibu Gavana wa Marsabit Solomon Gubo Riwe amesema kuwa shindano hili ambalo ni la kwanza kufanyika jimboni litasaidia wakaazi kuasi unyanyapaa kwa watu wanaoishi na ulemavu.Gubo ameelezea kuwa mashindano haya yatajenga umoja na mapatano baina ya Jamii zinazoishi Marsabit.