WAZAZI MARSABIT WAHIMIZWA KUTOWAFICHA WATOTO WALIO NA ULEMAVU WA KUPOOZA KWA UBONGO MAARUFU CELEBRAL PALSY.
November 4, 2024
Mikakati yote ya kuhakikisha kwamba mitihani ya kitaifa ya gredi ya sita KPSEA na ule wa kidato cha nne KCSE inayotajariwa kuanza jumaanne wiki ijayo katika kaunti ya Marsabit imekamilika.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ni kuwa ni jumla ya watahiniwa 8,383 wa shule za msingi ambao watakalia mtihani wa kitafa wa gredi ya sita KPSEA katika vituo vya mitihani 210.
Akizungumza na Radio Jangwani kwa njia ya simu, Magiri ametaja kwamba idadi ya wavulana bwatakao kalia mtihani huo ni 4,219 huku wasichana wakiwa ni 4,164.
Kuhusiana na mtihani wa kitaifa wa KCSE,Magiri amesema kuwa bodi ya mitihani nchini KNEC imeweka mikakati kabambe ya kuzuia wizi wa mitihani huku karatasi zote za watahiniwa zikijana na majina yao huku akifichua kuwa hakuna msimamizi yeyote wa mtihani atakayeruhusiwa kuwa na simu wakati wa mtihani.
Ili kuzuia visa vya kufungua karatasi zisizo sahihi,Magiri amebainisha kwamba karati zitakuwa na rangi tofauti.
Katika mtihani wa KCSE mwaka huu jumla ya wanafunzi 3,648 watakalia mtihani huo, 1,883 wakiwa ni wasichana huku 1,765 wakiwa ni wavulana katika vituo 48 vya mitihani.
Aidha mtihani wa KCSE mwaka huu utashuhudia idadi kubwa ya wanafunzi huria maarufu private candidates ambapo jumla ya wanafunzi 157 watakalia mtihani huo katika kauti ya Marsabit, 76 wakiwa ni wakike huku 81 wakiwa ni wakiume.