Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Caroline Waforo,
Wakaazi eneo la badassa eneo bunge la Saku kaunti ya Marsabit wamepongezwa kwa kudumisha amani. Hii ni baada yao kuwakamata vijana watatu usiku wa kuamkia leo na kuwawasilisha kwa idara ya usalama.
Watatu hao wanaodaiwa kutoka eneo bunge la Laisamis walipatikana usiku katika eneo la Badassa na baada iya kuhojiwa walidai kuwa walikuwa wakiwasaka mifugo wao waliopotea.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani naibu mwenyekiti wa kamati ya usalama katika kaunti ya marsabit Adan Chukulisa amepongeza jamii inayoishi Badassa kwa kitendo hicho anachokitaja kuwa ni kitendo cha utu.
Kwa upande wake Fredrick Lekesike ambaye ni mwanachama wa kamati ya usalama jimboni Marsabit amewatahadharisha vijana jimboni dhidi ya kujihusisha na visa vya wizi wa mifugo.
Kadhalika wamekosoa shambulizi la hivi majuuzi katika barabara ya Moyale-Marsabit ambapo basi la kampuni ya Salama lilivamiwa kwa miminiwa risasi pamoja na gari moja la kibinafsi aina ya land cruiser ambapo mtu moja alifariki.
Kwa pamoja wameitaka serikali kuhakikisha kuwa waliotekeleza uovu huo wanakamatwa na kuwajibishwa.
Kuhusiana na swala la maafisa wa akiba NPR viongozi hao wametoa wito kwa serikali kuongeza maafisa wa akiba NPR ili kusaidia maafisa wa polisi katika kuidumisha usalama hapa jimboni Marsabit.
Haya yanajiri huku OCS wa Marsabit Central Edward Mabonga akithibitishwa kuwa vijana hao wanaendelea kuziliwa katika kituo cha polisi cha Mrsabit huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini nia ya watatu hao kuwa katika eneo la Badassa majira ya usiku.