Idara ya vijana na michezo kaunti ya Marsabit yaaanda mafunzo ya siku mbili kwa vijana kuhusiana na jinsi ya kupata bima ili kutunza biashara zao, afya au hata bodaboda zao.
March 17, 2025
Na Samuel Kosgei
CHAMA cha kutetea maslahi ya walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri KUPPET tawi la Marsabit kimesisitiza kuwa kinaunga mkono mgomo wa walimu wa shule za upili unaoendelea kote nchini.Mwenyekiti wa chama hicho cha KUPPET hapa Marsabit Boru Adhi amesema kuwa muungano huo hautakubali walimu kurudi kazini hadi pale malengo na maombi yao yatakapotimziwa kikamilifu na mwajiri wake TSC.
Wakti uo huo wamewataka walimu wao wote wasifike shuleni na wasikubali kutishiwa kurejea kazini kabla maombi yao yaweze kuheshimiwa na serikali.
Kauli yake hiyo imesisitizwa na katibu wake Sarr Galgalo ambaye ametahadharisha walimu wakuu dhidi ya kutishia wala kudhulumu walimu ambao wamesusia kazi