Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
LICHA ya matukio ya kigaidi kupungua kwa kiasi kikubwa nchini kuna haja ya idara mbalimbali za serikali na hata washikadau wengine katika jamii kuzidi kushikamana na ili kumaliza kabisa kero ya ugaidi nchini.
Afisa kutoka kituo cha kutunga sera na mikakati ya kuzuia ugaidi nchini NCTC, Edwin Wameyo amesema kuwa juhudi zaidi bado inahitajika kuelimisha, kufahamisha na hata kuarifu jamii na vijana kuhusiana na hatari na athari za ugaidi nchini.
Amesema wengi wa vijana kutoka maeneo za mipakani na hujipata katika mitego ya walezi wa ugaidi kutokana na ukaribu na mataifa mengine na hata hali ya uchochole ambayo hufanya rahisi vijana kushawishika.
Wakati huo ameitaka jamii kuzidi kutoa habari na kuripoti matukio na hata watu ambao wanashuku kuendeleza mafunzo ya itikadi kali.
Anasema ni kupitia uwajibikaji wa jamii pekee ndipo itakuwa rahisi kuzuia na kudhibiti mipango na matukio ya kigaidi.