Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Kilo 521 na misokoto 386 ya bangi yenye Thamani ya shilingi milioni 12 imechomwa hii leo katika eneo la kutupa taka la Shegel kaunti ya Marsabit.
Bangi hiyo iliyonaswa kati ya mwaka 2019 hadi mwaka 2023 katika maeneo ya Turbi, North Horr, Loiyangalani pamoja na Marsabit ya kati imetekezwa kufuatia kutamatika kwa kesi zilizokuwa katika mahakama ya Marsabit.
Lita 24 za changaaa na aina mblimabli za pombe pia zilimwagwa.
Akiongoza shughuli hiyo kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau amesema kuwa katika siku za hivi karibuni idara ya usalama jimboni imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya.
Kamishna Kamau amesema kuwa serikali itahakikisha kuwa inakabiliana na walanguzi wote wa mihadarati na dawa za kulevya haswa kutumia mpaka wa Kenya na Ethiopia.
Vilevile ameweka wazi kuwa idara ya usalama imeimarisha doria mpakani mwa kenya na Ethiopia ili kuziba mianya yote ya ulanguzi wa mihadarati huku akitahadharisha jamii dhidi ya utumizi wa mihadarati.