IDARA YA ELIMU KATIKA KAUNTI YA MARSABIT YAWEKA MIKAKATI KABAMBE KUZUIA VISA VYA UCHOMAJI WA SHULE KUTOKEA HAPA JIMBONI.
September 12, 2024
NA HENRY KHOYAN
Jamii ya Rendile inayopatikana katika kaunti ya Marsabit pekee inalenga kufufua na kuimarisha mila na tamaduni zao kupitia kuonesha vyakula vya mbalimbali kitamaduni na mila zao za kutoka jadi.
Sherehe hiyo ya kipekee inatarajiwa kuanza Ijumaa tarehe 23 hadi 25 Agosti, ikiongozwa na shirika la Pastrolist People Initiative shughuli itakayofanyika katika mjini wa Loglogo kaunti hii ya Marsabit.
Hafla hiyo ya kitamaduni maarufu kama Rendille Food and cultural Festival itajumuisha matukio mbalimbali ya kiutamaduni ikiwemo upishi wa vyakula vya kienyeji, sherehe za kitamaduni, na mbio za ngamia maarufu kama camel Derby ambazo zitafanyika siku ya Jumapili ambao mshindi atatuzwa zawadi.
Hii ni fursa muhimu ya kuonyesha na kuenzi utajiri wa mila na desturi za jamii hiyo.
Stephen Basele ni Mkurugenzi katika shirika la hilo la Pastrolist People Initiative.
Basele amaesema lengo kuu la sherehe hiyo ni kufufua na kukuza mila ambazo zimeanza kudidimia.
Sherehe hii inatarajiwa kuleta jamii pamoja, huku akihimiza umuhimu wa kulinda lugha yao, ambayo imeonekana kupungua kwa kiasi kikubwa katika siku za hivi karibuni. Aidha, hatua hii inalenga kuhakikisha jamii hiyo inatambuliwa na kuenziwa kwa michango yao muhimu katika tamaduni na historia ya nchi.
Aidha Basele amesema kuwa wanatarajia wageni mbalimbali kushiriki katika sherehe hiyo, wakiwemo wawakilishi kutoka serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs), wanasiasa, na idara mbali mbali ya serikali.
Aidha Basele pia ameeleza kuwa jamii hiyo imealika jamii zote kutoka jimbo hili kushiriki katika sherehe hiyo ya kitamaduni. Sherehe hii inatarajiwa kuwa ya kipekee na ya kufana, ikijumuisha tamaduni mbalimbali na burudani za aina tofauti.