HEMORRHAGE (PPH) NDIO CHANZO KIKUU CHA VIFO MIONGONI MWA KINA MAMA WANAPOJIFUNGUA.
October 11, 2024
Na Isaac Waihenya,
Gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamed Ali ametuzwa kama Gavana mchapa kazi bora zaidi katika eneo la ukanda wa mashariki ya juu kwenye tuzo za ETA Awards mwaka wa 2024.
Kwenye hafla ya tuzo hizo iliyoandaliwa katika mkahawa wa kifari wa Samara mjini Machakos, pia Gavana Ali alichukua nafasi ya tatu kati ya Magavana 47 kwenye orodha ya magavana wachapakazi nchini kwa asilimia 68.63.
Kupitia mtandao wake wa kijamii wa X Gavana Ali ametaja kufurahishwa na kupata tuzo hilo huku akilitaja kama ni dhihirisho tosha kwa kazi anayowafanyia wananchi wa jimbo la Marsabit.
Aidha Gavana Ali amezidisha kusema kuwa atandelea kushikilia haki na uwazi katika utendakazi wake ili kuinua maisha ya wananchi wa jimbo hili.
Kadhalika ameutaja ushindi huo kuwa wa jimbo nzima la Marsabit na kuahidi kuendelea kuwahudumia wananchi kwa njia iliyo bora.