Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Afisa mmoja anayesimamia mitihani katika shule ya mseto ya Ruso iliyoko katika kaunti ndogo ya North Horr amekamatwa hii leo kwa jaribio la kuiba mtihani wa KCSE inayoendelea.
Akidhibitisha tukio hilo kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa mshukiwa alikamatwa akipiga picha mtihani wa hesabu na kutuma katika mitandao wa kijamii wa telegram.
Aidha Kimaiyo amesema kuwa afisa huyo amezuiliwa katika kituo cha polisi cha North Horr huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanyika.
Wakati huo kamanda Kimaiyo amewaonya wale wote walio na nia ya kuiba mitihani kukoma mara moja kwani serikali haitasita kuwakamata na kuwashitaki.
Mitihani hiyo imeingia siku yake ya pili wakiufanya somo la Hisabati paper 1 na Kiingereza (English comprehension paper)