Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Watoto walio kati ya umri wa miaka 8 hadi 17 huwa wanakumbana na changamoto ya kufanya maamuzi ambayo yatawajenga kimaisha jambo ambalo limetajwa kuwa linawaathiri kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa afisa anayesimamia mradi wa kituo cha maendeleo cha watoto (CDC) katika kanisa la E.A.P.C jimbo la Marsabit Mike Kinoti, ni kuwa watoto kati ya umri wa miaka 8 hadi 17, mara nyingi huwa wanafanya maamuzi mabaya ambayo yanawaadhiri katika maisha yao na kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi.
Akizungumza na idhaa hii, Kinoti amesisitiza ukaribu wa wazazi pamoja na wanao akisema kuwa utawasiaidia kujenga uhusiano mwema baina yao.
Kinoti amesema kuwa wazazi wanapaswa kuwatunza watoto walio katika kipindi cha kubalehe (Adolescent) ili kuwasaidia wajitambue na wajue wanachotakiwa kufanya, muda upi na katika mazingira yepi.
Hata hivyo Kinoti ametoa wito kwa wazazi kujukumika msimu huu wa likizo kwa kuhakikisha kuwa wanao wanaelimishwa ipasavyo kanisani na hata nyumbani ili kujenga jamii imara na yenye furaha.