Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
By Isaac Waihenya,
Wazazi wametakiwa kuwajukumisha watoto wao katika shughuli za nyumbani ili kuwaepusha kujiingiza katia uovu haswa wakiti huu wa msimu wa likizo ya Disemba.
Kwa mujibu wa viongozi wa kidini jimboni ni kuwa ni jukumu la wazazi kuhakikisha kwamba watoto wao wamo salama wakti huu wa likizo.
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa baraza za wahubiri katika kaunti ya Marsabit MPF Kasisi Said Lole na Sheikh Mohamed Noor wa msikiti wa jamia hapa mjini Marsabit, viongozi hao wamewarai wazazi kuwa karibu na wanao ili kuwaepusha na ngono za mapema, ukekekati, mihadarati na hata mimba za mapema.
Aidha wametoa wamewataka wazazi kuchunguza mitandao ya kijamii inayotumiwa na watoto wao na hata kutoa hamasa kwao.
Kuhusiana na swala la serekali kuangiza mahindi yaliyobadilishwa viinisaba GMO kutoka mataiafa ya nje viongozi hao wa kidini walikuwa na haya yakusema.