County Updates, Local Bulletins

Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Marsabit wanafaa kuwajibikia swala la usalama kikamilifu.

Muaniaji wa kiti cha ubunge katika eneo bunge la Saku mwaka wa 2022 Abduba Barille.
Picha:Hisani.

Na Waihenya Isaac,

Viongozi wa kisiasa katika kaunti ya Marsabit wanafaa kuwajibikia swala la usalama kikamilifu na kuhubiri Amani katika mikutano yao.

Hayo ni kwa mujibu wa muaniaji wa kiti cha ubunge katika eneobunge la Saku mwaka wa 2022 Abduba Barille.

Akizungumza na waandishi wa habari,Barille ametaja kuwa wanasiasa katika kaunti ya Marsabit wana ufahamu wa kutosha kuhuisana na yote ambayo yamekuwa yajikiri katika kaunti hii bila kuwajibika ila tu kunyoosheana lawama.

Barille na ambaye kwa wakti mmoja alitaja kuunga mkono Gavana wa kaunti ya Marsabit Mohamud Ali ameonekana kulenga vinginevyo huku akitaja kuwa Gavana Ali amefeli katika kuwahakikishia wananchi wa jimbo hili usalama wa kutosha na vilevile mazingira bora ya kufanyia Kazi.

Aidha Barille amewataka wa wananchi kutotumiwa vibaya na wanasiasa na badala yake kuwa na misimamo dhabiti haswa kuhusiana na swala la usalama jimboni.

 

Subscribe to eNewsletter