County Updates, Local Bulletins

Hisia mseto zazidi kuibuliwa kuhusiana na kauli ya Waziri wa Elimu Prof George Magoha kuwa ni lazima wazazi walipe karo ya shule ya muhula wa 3 la sivyo watoto warejeshwe manyumbani.

Waziri Wa Elimu Profesa George Magoha.
Picha:Hisani

By Samson Guyo,

Hisia mseto zinazidi kuibuliwa kuhusiana na kauli ya Waziri wa Elimu Prof George Magoha   kuwa ni lazima wazazi walipe karo ya shule ya muhula wa 3 la sivyo watoto warejeshwe manyumbani.

Baadhi ya wazazi waliozungumza na idhaa hii  mjini  Marsabit wametaja kuwa serekali haifai kulazimisha wazazi kulipa karo kwani idadi kubwa ya wazazi waliadhirika na janga la korona lilioadhiri kazi na hata biashara zao.

Baadhi yao wametaja kuwa Wizara ya elimu haifaia kuwaorodhesha wazazi kwa misingi ya  kipato chao.

Vilevile wamekashifu vikali kauli ya Waziri huyo wa elimu kuwa wazazi wengine kutoka kwa familia zinazojiweza   wamesusia kulipa karo kwa kisingizio cha kuadhiriwa na janga la korona wakiitaja kauli kama isiyo na misingi yeyote.

Akihutubu hiyo jana katika chuo kikuu cha JKUAT waziri Magoha aliwataka walimu wakuu kukagua kwa kina orodha ya wanafunzi na kubaini wanafunzi wanaotoka katika familia  maskini na wale walio na uezo wa kulipa karo na kuwachukulia hatua zinazofaa.

 

Subscribe to eNewsletter