County Updates, Diocese of Marsabit, Local Bulletins

Baadhi Ya Wachuuzi Mjini Marsabit Waandamana Hii Leo Wakilalamika Kuhusu Nyongeza Ya Kodi Kutoka Shilingi 20 Hadi 100.

Baadhi Ya Waachuzi Kutoka Mjini Marsabit Walipofika Katika Ofisi Za Mkuu Wa Manisipaa Ya Marsabit Kuwasilisha lalama zao.
Picha; Mark Dida

By Mark Dida & Silvio Nangori

Wachuuzi kutoka kaunti ya Marsabit eneo Bunge la Saku wameandamana hii leo  wakilalamika kuhusu nyongeza ya Kodi kutoka shilingi 20 Hadi 100.

Miongoni mwa malalamishi yao ni kwamba wanaokusanya Kodi wanafanya shughuli hiyo kwa ubaguzi jambo ambalo wengi wanadai ni hali ya kudhulumiwa ikizingatiwa kwamba wao ni wafanyibiashara wadogo.

Kwa upande wake mwenye kiti wa chama cha manisipaa Roba Sereqa amekanusha madai ya wafanyakazi hao kubaguliwa  akisema Kuwa Ni uchochezi Na semi za uongo.

Baadhi Ya Waachuzi Kutoka Mjini Marsabit Walipofika Katika Ofisi Za Mkuu Wa Manisipaa Ya Marsabit Kuwasilisha lalama zao.
Picha; Mark Dida

Akizungumza akihutubia wafanyibiashara hao Roba amedai kwamba wanaotozwa Ushuru ya Shilingi mia Moja ni Wachuuzi huku walio na vibanda mahala pamoja bila kuzunguka wanatozwa shilingi Ishirini.

Aidha ameongeza kwamba Mwezi wa Nne hadi disemba mwaka uliopita hawakutoza mfanyibiashara yeyote hata senti moja kwa ajili ya hali ngumu ya kupambana na Virusi vya korona.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter