County Updates, Local Bulletins

Wauguzi Na Matabibu Katika Hospitali Za Umma Kaunti Ya Marsabit Wametangaza Kuwa Wataendelea Na Kazi.

Picha; Hisani

By Mark Dida.

Huku Mgomo Wa Wauguzi Na Matabibu Ukiendelea Kote Nchini, Wauguzi Na Matabibu Katika Hospitali Za Umma Kaunti Ya Marsabit Wametangaza Kuwa Wataendelea Na Kazi.

Katika Hospitali Ya Rufaa Ya Marsabit, Wauguzi Na Matabibu Wanaendelea Kuwahudumia Wagonjwa, Huku Afisa Mkuu Mtendaji Wa Hospitali Ya Marsabit Liban Wako Akisema Mapendekezo Waliyotoa Kwa Kaunti Hii Yameafikiwa.

 

Liban Wako Afisa Mkuu Mtendaji Wa Hospitali ya Rufaa Ya Marsabit. Picha ; Mark Dida

Liban Amesema Kuwa Zoezi La Kuwapima Watu Juu Ya Ugonjwa Wa Covid -19 Linaendelea Vyema Kufikia Sasa, Akiongeza Kuwa Ipo Haja Ya Watu Kujitokeza Kufanyiwa Vipimo Hivyo Ili Ibainike Iwapo Wameambukizwa Au La.

Wakati Uo Huo, Liban Amefichua Kuwa Idadi Ya Wagonjwa Wanaotafuta Matibabu Imepungua Tangu Kuchipuka Kwa Janga La Covid 19, Kutoka Wagonjwa 200 Hadi 100 Kwa Siku.

Aidha, Amesema Kuwa Watu Wengi Wanadhani Wataambukizwa Wakati Watatembelea Vituo Vya Afya Kwa Matibabu Baada Ya Marsabit Kuripoti Zaidi Ya Visa 30 Vya Wahudumu Wa Afya Kuugua Covid-19.

Leave a Comment

Your email address will not be published.

Subscribe to eNewsletter