County Updates, Local Bulletins

Wafanyikazi Katika Sekta Ya Uchukuzi Kaunti Ya Marsabit Walalamikia Kudorora Kwa Biashara Baada Ya Sheria Mpya Za Korona.

Picha; Hisani

By Adho Isacko.

Wafanyikazi Katika Sekta Ya Uchukuzi  Kaunti Ya Marsabit Wamelalaimikia Kile Walichokitaja Kuwa Kudorora Kwa Biashara Baada Ya Sheria Mpya Za Kuzui Kusambaa Kwa Virusi Vya Korona.

Serekali Kupitia Wizara Ya Afya  Iliagiza Magari Yote Ya Usafiri Kupunguza Idadi Ya Abiria Kama Njia Mojawapo Ya Kuzua Msambao Wa Homa Hatari Ya Korona.

Kwa Mujibu Wa Mhudumu Wa Kampuni Ya Meiso Juma Ahmed Ni Kuwa Agizo Hilo Ni Pigo Kwa Biashara Yao Haswa Wakati Huu Watu Wengi Wanasafiri Maeneo Mbali Mbali Kwa Shamrashamra Za Krismasi Na Mwaka Mpya.

Aidha, Amesema Wasafiri Wengi Wamelazimika Kuahirisha Safari Zao Kwa Ajili Ya Kukosa Mbini Za Usafiri.

Juma Ameitaka Wizara Ya Afya Katika Kaunti Ya Marsabit Kurejelea Shughuli Ya Upimaji Joto Wa Wanaosafiri

Kwa Upande Wake Mhudumu Wa Nanyuki Cabs Jackson Mwenda Amesema Kuwa Wasafiri Wamepungua Mno Msimu Huu Wa Krismasi Ikilinganishwa Na Miaka Iliyopita.

Mwenda Amelaumu Mkurupuko Wa Janga La Covid-19 Kwa Kuchangia Kulemaa Kwa Uchumi Kando Na Kupelekea Watu Wengi Kupoteza Ajira Zao.

Subscribe to eNewsletter