Local Bulletins

Zoezi la kuhesabu wafanyakazi wote wa kaunti lakamilika idadi kamili ikitolewa karibuni.

Na mwandishi wetu

Serikali ya kaunti ya Marsabit imekamilisha zoezi la kuhesabu wafanyakazi wote wa kaunti na idadi kamili iliyochujwa na kufanyiwa marekebisho itatolewa kabla ya mwezi wa nne kukamilika.

Naibu katibu wa kaunti ambaye pia naibu mkuu wa wafanyakazi Doti Tari amesema kuwa lengo kuu la zoezi hilo ni kuimarisha huduma na shughuli za kiserikali.

Zoezi hilo la kuanza kuhesabu wafanyakazi wa serikali ya kaunti ilifanyika mwanzo mwezi Novemba mwaka jana wakianza na eneobunge la Saku zoezi hilo pia amesema limefanyika katika maeneobunge mengine ya Laisamis, Moyale na North Horr.

Zoezi hilo mwaka jana anasema lilitatizwa na ukosefu wa fedha kufadhili shughuli hiyo.

Doti ameongeza kuwa lengo la kufanya hesabu hiyo ni ili kujua idadi kamili ya wafanyakazi wanaofika kazini na kuhakikisha kuwa kazi ya mtu inaendana na ujuzi na taaluma aliyosomea.

Anasema kupitia hilo watazuia kuchanganya taaluma aliyosomea mtu na kazi anayofanya kwa sasa.

Orodha mpya ya waajiriwa itakapotolewa anasema itasaidia kuyaondoa majina ya watu waliofariki au hata kustaafu kati ya nyingine.

Subscribe to eNewsletter