Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na JB Nateleng,
Zaidi ya shule 25 katika kaunti ya Marsabit zitanufaika na mradi wa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi ambao utafadhiliwa na shirika la shirika la Wilderness Conservation Center (WCC).
Kwa mujibu wa mwanzilishi wa shirika hilo Albert Borges ni kuwa wanapanga kuwaelimisha na kuwawezesha wanafunzi kwa kutoa mafunzo muhususi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ambayo yatasaidia katika kuimarisha na kuboresha mazingira.
Akizungumza na wanahabari Albert amesema kuwa wamelenga wanafunzi kwa sababu wao ndio viongozi na kielelezo cha jamii ya kesho hivvo kuwarai walimu, wazazi pamoja na wanafunzi kushirikiana kwa pamoja na kukumbatia mradi huu ambao ameutaja kuwa utasaidia katika kupunguza makali ya kiangazi sawana kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Aidha Albert ameelezea kuwa japo mradi huu utawajenga wanafunzi kwa kuwahamasisha kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, kuna haja ya washikadau zaidi kuweza kushirikiana ili kufanikisha na kuiboresha mradi huo kwa manufaa ya jamii.
Kauli yake imeungwa mkono na msimamizi mkuu wa KWS Agostin Ajuoga ambaye amesema kuwa hatua hii itasaida watoto kuwa mabalozi wa kutunza misitu na huenda ikaimarisha ulinzi wa misitu na wanyama pori katika jimbo la Marsabit.