KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Wizara zapata nyongeza ya shilingi bilioni 113 katika bajeti ya ziada.
Rais William Ruto ametia saini Bajeti ya Ziada ya Pili ya mwaka wa fedha 2024/25 ambayo itatenga Ksh.113 bilioni zaidi kwa wizara mbalimbali.
Kama inavyoonekana katika Mswada wa Ugawaji wa Fedha wa Ziada, ambao tayari umeidhinishwa na Bunge la Kitaifa, mgao huu utashughulikia pengo la kifedha lililopo katika sekta mbalimbali.
Ongezeko hili la mgao kwa wizara sasa limepanda hadi Ksh.2.3 trilioni kutoka shilingi trilioni 2.2 zilizotengwa katika Makadirio ya Awali ya Bajeti ya Ziada ya kwanza.
Sekta nyingine muhimu zitakazonufaika na Makadirio ya Bajeti ya Ziada ya pili ni pamoja na juhudi za kukabiliana na ukame ambazo zitapokea Ksh.5 bilioni.
Sekta ya barabara itapokea Ksh.16 bilioni, Ksh.4.6 bilioni kwa Wizara ya Utalii.
Mswada huo pia umetenga Ksh.18 bilioni kwa Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) ili kushughulikia upungufu wa fedha za bima, kupandisha vyeo kwa walimu, na kuangaziwa upya kwa mishahara ya wafanyakazi.