Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Samuel Kosgei
Kamati ya bunge kuhusu fedha katika bunge la kaunti ya Marsabit imesema iko mbioni kwa sasa kukamilisha mchakato wa bajeti ili kuwasilishwa bungeni kujadiliwa na kupitishwa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni MCA wa Korr/Ngurnit Daud Tomasot amesema kuwa mchakato huo kwa sasa upo katika hatua ya marekebisho na wanaweza kujadili na kupitisha terehe 30 mwezi huu wa sita.
Ameambia radio jangwani kuwa makadirio ya bajeti katika mwaka wa kifedha mwaka wa 2025/26 ni shilingi bilioni 9.8 na huenda ikapanda hadi sh.10bn kutokana na ripoti kuwa Marsabit huenda ikapata nyongeza kutoka serikali ya kitaifa.
Kwenye makadario hiyo kama iliyovyokuwa mwaka jana idara ya afya ndio imetengewa mgao mkubwa wa Zaidi ya asilimia 30 ya bajeti yote kutokana na upana wa idara na muundo msingi wake, wizara ya kilimo, ufugaji na uvuvi pia imetengewa mgao mkubwa kwenye makadirio ya mwaka mpya wa kifedha.