Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Moses Sabalua,
Wito umetolewa kwa vijana katika kaunti ya Marsabit kujiunga na utawa.
Wito huu umetolewa na Fransinsca Diboya Matacho ambaye ni mwanafunzi katika kikundi cha Little Sisters of Saint Francis ambaye anaendleza masomo ya utawa.
Akizungumza hiyo jana jumapili katika kanisa katoliki la mtakatifu Maria Consolata jimboni Marsabit, Diboya amesema kuwa ni nadra kupata wito huo haswa katika kaunti ya Marsabit huku akiwashawishi vijana kuwa mstari wa mbele na kujiunga na utawa pamoja na upadre.
Vile vile Diboya ameonyesha furaha yake ya kujiunga na utawa akiwataka wazazi kuitikia wito wa wanawao ambao wangetaka kujiunga na utawa ama upadre.