Local Bulletins

Wito watolewa kwa wazazi kushirikiana na walimu kwenye vita dhidi ya mihadarati.

Na Muchai Joseph

Wito umetolewa kwa wazazi katika kaunti ya Marsabit kushirikiana na walimu kwenye vita dhidi ya utumizi wa Mihadarati.

Akizungumza na shajara ya Radio Jangwani mwanaharakati wa kukabiliana na mihadarati katika kaunti ya Marsabit Fredric Ochieng amesema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwazomea walimu pindi watoto wao wanapopatikana wakitumia mihadarati shuleni.

Ochieng aidha amesema kuwa uraibu na matumizi ya mihadarati shuleni na kwenye jamii huanzia nyumbani miongozni mwa watu walio karibu na watoto na mwishowe kuwafundisha watoto utuamizi wa dawa hizo.

Wakati uohuo mwanaharakati huyo amesema kuwa imewabidi yeye na kikosi cha kukabiliana na dawa za kulevya kubadilisha mbinu za kupambana na mihadarati kwa kutembelea shule mbalimbali ili kuwafundisha wanafunzi kuhusianana na madhara ya mihadarati wanagali wadogo.

Subscribe to eNewsletter