Local Bulletins

Wito watolewa kwa waendeshaji bodaboda mjini Marsabit kuwa makini wanapotumia barabara msimu huu wa mvua.

Na Moses Sabalua,

Waendeshaji bodaboda pamoja na wakaazi mjini Marsabit wametakiwa kuwa makini wanapotumia barabara msimu huu wa mvua.

Hii ni baada ya kifo cha mwendeshaji mmoja wa bodaboda kupoteza maisha mnamo siku ya Jumatatu baada ya kuhusika katika ajali.

Akizungumza na Shajara ya Redio Jangwani kamanda wa trafiki katika kaunti ya Marsabit Jacob Kiprop amewataka waendeshaji bodaboda kuvalia sare maalum wanapoendesha bodaboda kwa minajili ya usalama wa barabarani.

Kiprop amewahakishia wanabodaboda usalama wao barabani hata baada ya kisa cha wizi wa bodaboda kuripotiwa siku chache zilizopita.

Wakati uo huo Kiprop amewaonya waendeshaji bodaboda dhidi ya kufanya kazi baada ya saa sita ili kuimarisha usalama wao.

Kamand huyo wa trafiki ametoa onyo kali kwa waendeshaji boda boda ambao hawajatimiza umri akisema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao iwapo watakapokamatwa.

Subscribe to eNewsletter