Local Bulletins

Wito watolewa kwa viongozi nchini kuasi siasa na badala yake kuangazia maswala yanayowaadhiri wananchi……

Na Isaac Waihenya,

Wito umetolewa kwa viongozi nchini kuasi siasa na badala yake kuangazia maswala yanayowaadhiri wananchi.

Kwa mujibu wa Sheikh Bashir Somo ni kuwa viongozi wamewatelekeza wananchi na badala yake kuanza kurindima siasa za mwaka wa 2027 kuliko kuangazia maendeleo.

Akizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani, Sheikh Bashir ameweka wazi kwamba wananchi wa jimbo la Marsabit na maeneo mengine ya kaskazini mwa nchi wanakabiliwa na hatari ya ukosefu wa chakula kutokana na hali ya kiangazi huku viongozi wakiendeleza siasa.

Aidha Sheikh Bashir ametoa wito kwa wananchi walio na uwezo kuwajali wasio na uwezo huku akiyarai mashirika ya kijamii jimboni kuingilia kati ili kutatua hali.

Kuhusiana na matokeo ya uchaguzi wa AUC uliokamilika hivi maajuzi,kiongozi huyo wa kidini amemtaka kinara wa ODM Raila Odinga alipoteza kwenye uchaguzi huo kushirikiana na rais Ruto Wiliam Ruto katika kuwafanyia kazi wananchi ili kuboresha na kuinua uchumi wa taifa.

Subscribe to eNewsletter