Local Bulletins

Wito watolewa kwa vijana nchini kutokubali kutumika kuzua vurugu

Na Isaac Waihenya,

Wito umetolewa kwa vijana nchini kusima kidete na kutetea haki zao kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Ni wito ambao umetolewa na mshirikishi wa shirika la Initiative for Progressive Change IFPC katika kaunti ya Marsabit Hassan Mulata.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya kipekee, Mulata amewataka vijana kutokubali kutumika kuzua vurugu na badala yake wawe katika mstari kwanza kusukumiz aajenda zao.

Aidha Mulata amekemea mauaji ya bwanablogu Albert Ojwang pamoja na vijana wengine nchini huku akitoa wito kwa idara husika kuhakikisha kwamba haki inapatikana kwa waadhiriwa.

Mulata pia ametoa wito kwa vijana wa Marsabit kushikana bila kujali dini wala kabila na kuandaa vikao vya kuwawajibisha viongozi kuhusiana na maswala yanayowahusu kabla ya kuamua kuandaa maadamano.

Kuhusiana na swala la uwepo wa bunge la vijana katika maeneo bunge yote maanne ya jimbo hili, haswa baada ya kubuniwa kwa bunge la Moyale Youths Assembly, Mulata amewataka vijana wa maeneo bunge ya North Horr na Laisamis kuwa na subira, mikakati inapoangaziwa kuhusiana na namna pia maeneo hayo yatapata bunge hilo.

Subscribe to eNewsletter