Local Bulletins

Wito watolewa kwa serekali kuu na serekali ya kaunti ya Marsabit kuharakisha mchakato wa kusajili ardhi ya Loiyangalani.

Na JB Nateleng,

Wito umetolewa kwa serekali kuu na serekali ya kaunti ya Marsabit kuharakisha mchakato wa kusajili ardhi ya Loiyangalani ili kuwapa wakazi wa eneo hilo uhuru wa kumili ardhi yao kisheria.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa shirika la Wongan Women Initiative Teresalba Sintian ni kwamba ardhi ya Loiyangalani imekaa kwa muda bila usajili jambo ambalo linatatiza jamii.

Akizungumza na idhaa hii kwa njia simu, Teresalba amedokeza kwamba itakuwa ni afueni kwa wakaazi wa Loiyangalani wakati ambapo usajili wa ardhi yao utakapowekwa rasmi katika gazeti la serekali.

Kadhalika Teresalba ameelezea kwamba kufikia sasa jamii zinazoishi Loiyangalani zimeweka mikakati yote hitajika ili kufanikisha usajili wa ardhi hiyo.

Aidha Teresalba amewataka viongozi kuunganisha wakazi wa eneo hilo kwa kuwapa elimu sahihi kuhusu umuhimu wa usajili wa ardhi.

Teresalba ametaja fedha kuwa changamoto haswa ikizingatiwa kwamba usajili wa ardhi unahatua nyingi ambazo zinayataka mashirika yasiyo ya kiserekali kuungana pamoja ili kurahisisha mchakato huo.

Subscribe to eNewsletter