Local Bulletins

Wito watolewa kwa mashirika mbalimbali jimboni Marsabit kuhusisha jamii katika miradi ya maendeleo.

Na JB Nateleng,

Jamii inafaa kuhusishwa katika kila mradi ambao unafaa kutekelezwa katika maeneo yao ili kupunguza visa vya kuwa na mradi ambao unakosa kuafikia masuala yanayoiadhiri jamii.

Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu katika idara ya maliasili na wanyama pori, kaunti ya Marsabit Bi. Pauline Marleni.

Akizungumza kwenye warsha iliyowaleta pamoja washikadau kutoka idara mbalimbali katika kaunti ya Marsabit, iliyofadhiliwa na shirika la la Wilderness Conservation Center (WCC) Bi Pauline amesema kuwa ni wajibu wa kila shirika kuhakikisha kuwa limezingatia maoni na maelezo ya jamii kabla ya kuanzisha mradi wa aina yeyote ili kupata uungwaji mkono wa jamii.

Afisa huyu ameelezea kuwa ni wakati mwafaka sasa wa kusaka suluhu la mambo yanayoadhiri jamii haswa wakati huu ambapo wakazi wanazidi kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi.

Huku akiunga mkono mradi huu wa kuanzisha mafunzo ya mabadiliko ya tabia nchi kwa wanafunzi jimboni Marsabit, Marleni amewataka wakuu wa shule kuweza kujitolea na kuhakikisha kuwa wamejitwika majukumu ya kuendeleza mradi huu ili kufikia malengo tarajiwa.

Subscribe to eNewsletter