Wizara ya afya Marsabit ndio iliyotengewa mgao mkubwa, Zaidi ya 30% kwenye makadirio wa kifedha 2025/26
June 20, 2025
Na Samuel Kosgei
WAZIRI wa usalama Kipchumba Murkomen ameahidi kuwa serikali itafanikisha kuondolewa kwa wakimbizi wa ndani walio kaunti hii ya Marsabit ili kurejeshwa makwao na kuendeleza maisha yao ya hapo awali.
Akizungumza hii leo kwenye kikao cha usalama kwa jina jukwaa la usalama Murkomen amesema kuwa ni aibu kwa wakimbizi hao kusalia kwenye kambi zao licha ya hali ya usalama kurejea kaunti ya Marsabit.
Amesema kuwa serikali ya kitaifa itashirikiana na serikali ya kaunti ili kuondolewa kwa wakimbizi hao ambao wamesalia hapo kwa muda mrefu.
Waziri Murkomen pia amesema serikali hii mbioni kusaka pesa ambazo zitatumika kukamilisha kubuniwa kwa kaunti ndogo zote mpya ambazo zimeahidiwa kaunti ya Marsabit na serikali iliyopita.
Murkomen amesema kuwa idara ya utawala inahitahi zaidi ya shilingi bilioni 2.5bn ili kutimizwa kwa uzinduzi wa kaunti hizo ndogo ikiwemo Illeret, Korr, Shurr, Sagante Jaldesa, Golbo, Uran kati ya nyingine ambazo zilitangazwa kwenye gazeti rasmi la serikali.
Murkomen aidha ameonya maafisa wa usajili wa vitambulisho ambao wanazidi kuhangaisha wananchi ambao wanasaka huduma za kitambulisho. Ameonya pia machifu na maafisa wa kutoa kitambulisho ambao watapitia njia za mkato na kilaghai kutoa kitambulisho.
Wakati uo huo ameonesha masikitiko kuwa kwa muda licha ya kaunti ya Marsabit kutengewa miradi za serikali kwenye bajeti bado miradi hiyo haitekelezwi kutokana na maeneo kame kutengwa na maafisa waliofaa kufikisha maendeleo mashinani.
Amerai gavana wa Marsabit na wabunge kufuatilia kwa karibu miradi ya Marsabit iliyo kwenye bajeti mpya ili wananchi wafurahie pia matunda ya serikali ya sasa.