Local Bulletins

Wazee katika kaunti ya Marsabit watakiwa kueeneza habari ya umuhimu wa Amani haswa kwa vijana.

Na Isaac Waihenya,

Wazee pamoja na viongozi wa kijamii katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuhakikisha kwamba wameeneza habari ya umuhimu wa Amani haswa kwa vijana.

Kwa mujibu wa kamishina wa kaunti ya Marsabit James Kamau ni kuwa vijana wanafaa kuelimishwa kuhusiana na umuhimu wa Amani sawa na madhara ya ukosefu wa Amani.

Akizungumza wakati wa mkao uliowaleta pamoja viongozi wa kijamii katika kaunti ya Marsabit sawa na viongozi wa usalama, kamishina Kamau amelitaja jukumu la kuidumisha Amani na kuhubiri uiano kwa la kila mkaazi wa jimbo hilo.

Kamishina Kamau amewaonya wale ambao amewataja kwamba hawafurahii wakati kaunti ya Marsabit iko na Amani huku akisema kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kuhusiana na kisa cha mauaji ya mwanabodaboda aliyeuwawa siku chache zilizopita katika eneo la Harobota vyungani vya mji wa Marsabit, kamishina Kamau amelaumu jamii kwa kutotoa taarifa muhimu zitakazosaidia katika kuwakamata waliotekeleza uovu huo.

Kadhalika kamishina Kamau ameonya dhidi ya kueneza uvumi unaoweza kuchochea uhasama kati ya jamii zinazoishi katika kaunti ya Marsabit.

 

Subscribe to eNewsletter