Local Bulletins

Wazazi wa shule ya upili ya El-Mosaretu girls wamkataa mwalimu mkuu mpya aliyehamishiwa shuleni humo….

Na Waandishi wetu,

Wazazi wa shule ya upili ya El-Mosaretu girls iliyo eneo la Loyangalani eneo bunge la Laisamis kaunti ya Marsabit wamejitokeza na kupinga hatua ya tume ya kuajiri walimu nchini TSC kubadilisha uongozi wa shule hiyo.

Wazazi hao wameelezea kutofurahishwa kwao na maamuzi ya kumhamisha hadi shule hiyo mwalimu Madina Marme ambaye alikuwa mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Maikona girls, ambaye pia alikataliwa na wazazi wa shule ya upili ya Sasura girls mwezi jana wakisema kuwa hawakuridhishwa na maamuzi hayo na kuitaka idara ya elimu jimboni kutoa maelezo zaidi kuhusiana na zoezi hilo.

Wakizungumza na meza ya habari ya Radio Jangwani wazazi hao wamesema kuwa wangetaka jamii nzima ya Loiyangalani kuhusishwa wakati ambapo maamuzi ya usimamizi wa shule hiyo yanajadiliwa na kufanyika.

Wameitaka Tume ya kuajiri walimu nchini (TSC) kuweza kumpa muda alikuwa mwalimu mkuu wa shule hiyo ili kujenga na kuimarisha msingi wa shule ya upili ya EL-Mosaretu girls kwa ajili ya manufaa ya jamii ya Loiyangalani.

Kwa upande wake Stephen Nakeno ambaye alikuwa mwakilishi wadi wa eneo hilo amesema kuwa ni sharti TSC iweze kuhusisha na kusikiza malalamishi ya wanaLoiyangalani kabla ya kufanya maamuzi ya kumleta mwalimu huyo katika shule hiyo.

Subscribe to eNewsletter