KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Muchai Joseph
Wazazi karika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwachunga wanao wasije wakapata uzito wa kupindukia. Akiongea na kituo hiki naibu mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya SKM Ruth Lekesike amewataka wazazi kuhakikisha kuwa wanao wanapata muda wa kucheza na kufanya mazoezi ili kuwakinga na unene uliopindukia.
Wakati uohuo Bi Lekesike amewataka wanafunzi kujihusisha na shughuli za kuchangamsha viungo vya mwili ili kuboresha afya kwani muda mwingi watoto wengi wamekuwa wakijihusisha na kutazama runinga na simu za mkononi swala linalowanyima nafasi ya kufanya zoezi muhumu kwa afya.
Haya yanajiri huku uchunguzi ukionesha kuwa kwa sasa watoto wengi humu nchini wana unene wa kupindukia yani ujalivu.