Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na Isaac Waihenya,
Watoto kumi na watatu wa shule ya msingi ya Moite iliyoko wadi ya Loiyangalani kaunti ya Marsabit wanaendelea kupokea matibabu baada ya kupimwa na kukutwa na ugonjwa wa Sarua yaani Measles.
Kwa mujibu afisa wa afya katika kaunti ndogo ya Laisamis Yusuf Galmogle ni kuwa sampuli tatu zilitumwa kwa maabara ya KEMRI mapema wiki hii ambapo matokeo yailionyesha kwamba watoto hao walikuwa wanaugua maradhi ya Sarua.
Akizungumza na idhaa hii kwa njia ya simu Galmogle amesema kuwa kwa sasa watoto wanaendelea kupokea matibabu chini ya uangalizi wa muunguzi wa zahanati ya Moite.
Aidha Galmogle ameweka wazi kuwa idara ya afya imeweka mikakati kabambe kukabiliana na hali hiyo huku akiwahakikishia wananchi kuwa chanjo ya ungojwa huo inapatikana katika zahanati ya Moite.
Kwa upande wake MCA wa wadi ya Loiyangalani Daniel Emojo Musa amesitiza haja ya kuwachanja watoto katika eneo hilo ili kuzuia ugonjwa huo.