Itakua vigumu kwa rais Ruto kupata muhula wa pili iwapo hatatimiza ahadi zake
May 12, 2025
Na JB Nateleng
Ili kujenga kanisa lenye matumaini ni Lazima wakristu waweze kushirikiana kwa kueneza neno la Mungu
Haya yamewekwa wazi na watawa wa shirika la evangelizing sisters of Mary jimboni Marsabit wakisema kuwa lengo la kanisa ni kuwaleta wakristu pamoja na kuwafanya waishi kwa upendo.
Watawa hawa wamesema kuwa ili kuwepo na umoja kanisani ni jukumu la Kila mkristu kujumuika na wakristu wenzao kwa kuhudhuria vikao vya jumuiya, na kusali pamoja.
Matamshi yao yanajiri baada ya kanisa katoliki kusherehekea wiki ya masista watawa wa katoliki, wakisema kuwa wanajukumika katika kuhakikisha kuwa injili imeenea kote haswa katika Jimbo la Marsabit huku wakipongeza juhudi ya Askofu, mapadri pamoja na walei jimboni kuhakikisha kuwa injili imefika mashinani.
Wametaja changamoto za lugha kuwa kizingiti Cha kueneza injili jimboni ila wanajaribu kuwatumia wakalimani ambao wamewasaidia pakubwa katika kueneza injili.