KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Mwandishi Wetu
Watu wanne wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa la kuendesha biashara ya kuuza vileo bila leseni mjini Marsabit.
Wanne hao ni kati ya watu watano waliokamatwa hapo jana Alhamisi kufuatia msako dhidi ya pombe haramu na mihadarati unaoendeshwa na mamlaka ya kitaifa ya kudhibiti pombe na dawa za kulevya NACADA pamoja na mamlaka ya kukadiria ubora wa bidhaa nchini KEBS.
Wanne hao Martin Mwenda, Lydia Mwende, Mirrriam Kibiritho pamoja na Luswet Sharon wanakabiliwa na kosa la kuendesha biashara hiyo bila leseni ya kuuza vileo ya mwaka 2025 huku pia wengine wakikabiliwa kosa la pili la kuuza vileo kutumia chupa zilizo chini ya mililita 250.
Wanne hao wamefikishwa mahakamani leo Ijumaa mbele ya hakimu mwandamizi Simon Arome ambaye amewapiga faini ya shilingi 30,000 au kifungo cha miezi 6 huku wengine wakiongezewa faini ya shilingi 1,000 au kifungo cha siku saba kwa kosa la pili.
Mahakama pia imeamuru mshukiwa wa tano Caroline Mwende kukamatwa baada yake kukosa kujiwasilisha mahakamani leo hii.
Msako huo bado unaendelea.