Wizara ya afya Marsabit ndio iliyotengewa mgao mkubwa, Zaidi ya 30% kwenye makadirio wa kifedha 2025/26
June 20, 2025
Na Caroline Waforo,
Wanawake wajane na wanao walea wanao pekee wamelalama kudhulumiwa na kubaguliwa katika jamii katika kaunti ya Marsabit.
Haya yamebainika wakati wa kikao cha kukusanya maoni kuhusu ongezeko la visa vya dhulma za kijinsia na mauaji ya wanawake kinachoendeshwa na jopo maalum la kuchunguza visa hivi liloloteuliwa na Rais William Ruto miezi mitatu iliyopita kufuatia ongezeko la visa vya mauaji ya wanawake nchini.
Wakizungumza katika kikao hicho baadhi ya waathiriwa wamelalama kuwa wanabaguliwa katika jamii huku wakiitaka serikali kuu kuingilia kati na kukomesha unyanyapaa uliopo.
Haya yanajiri siku chache tuu baada ya serikali kukusanya idadi ya wanawake wajane na wanao walea wanao pekee kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi.