Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Joseph Muchai,
Siku moja bada ya ulimwengu kusherehekea siku ya kimataifa ya akina baba maarufu Father’s Day wakaazi wa Marsabit mjini wametoa maoni yao kuhusu siku hiyo.
Baadhi ya waliozungumza na Shajara ya Radio Jangwani wameelezea kuwa wanaume wengi hawakuhisi kutambuliwa kama baba katika siku hiyo.
Aidha wengine wao wanahisi kuwa wanaume hutelekezwa kimaslahi na jamiii tangia utotoni kutokana na dhana ya jamii kuwa mwanaume huzaliwa akiwa na uwezo hivyo basi hafai kuwezeshwa.
Wametoa hisia mseto kuhusiana na akinadada waliosherekea siku ya akina baba duniani kwenye mitandao huku wakihisi kuwa ni dharau dhidi ya wanaume waliozaa watoto nao na pia ni aibu kwa jamii.
Siku ya akina baba duniani husherehekewa kila jumapili ya tatu ya mwezi juni kila mwaka. Huwa inasherehekewa kwa kadi, zawadi, kula kwa pamoja na familia pamoja na shughuli zingine.