Wanafunzi waliokamilisha elimu watakiwa kuwa na subira kuhusu kupokea vyeti vyao vya masomo.
March 25, 2025
Na caroline Waforo
Wataalam wa kisaikolojia pamoja na wazazi watahusishwa katika maamuzi ya taaluma yatakayofanywa na wanafunzi chini ya mtaala wa umilisi CBC.
Hayo ni kulingana na mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit Peter Magiri ambaye amezungumza wakati wa kikao cha majadiliano kuhusu ubora wa elimu chini ya mtaala huo siku ya Jumatatu.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya upili ya Moi Girls killiongozwa na idara ya elimu ya msingi na kuhusisha maafisa kutoka KICD, KNEC, TSC, waakilishi wa walimu, wazazi pamoja na viongozi wa kidini.
Vile vile ameweka wazi kuwa mikakati itawekwa kufanikisha mpito kwa wanafunzi wa gredi ya 9 hadi gredi ya 10.
Kwenye kikao hicho lalama zimeibuliwa kuhusiana na upungufu wa vitabu vya mtaala huu wa CBC mkrugenzi huyu wa elimu Peter Magiri akisema kuwa ni swala ambalo limeshughulikiwa na serikali kupitia wizara ya elimu.
Mazungumzo haya yanafanyika katika kaunti zote 47 nchini.