Local Bulletins

Wanaonufaika na mpango wa Inua Jamii kupokea fedha za mwezi Februari kabla ya mwisho wa wiki hii.

Na Caroline Waforo.

Waonufaika na mpango wa Inua Jamii katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kutembela afisi za idara ya Inua jamii iwapo wanapitia changamoto zozote baada ya serikali ya Kenya kuhamisha mpango wa pesa zote za Inua jamii kwenye M- PESA.

Haya ni kulingana na mshirikishi wa idara ya Inua jamii katika kaunti ya Marsabit Vincent Musee ambaye amesema kuwa mpango wa kuhamisha fedha hizi hadi kwenye mfumo wa E-Citizen uliletwa ili kuwapunguzia mzigo mzito wanaonufaika na mpango huo.

Aidha Musee amekanusha madai kuwa fedha za wanaonufaika na mpango huo watazipoteza iwapo zitakaa kwa muda wa miezi mitatu bila kutolewa.

Vile vile Musee ameweka wazi ni katika mazingira yepi ambapo fedha zinaweza kurejeshwa kwa akaunti ya serikali iwapo anayenufaika hajachukua fedha zake.

Kadhalika Musee ameweka wazi kuwa usajili wa watu wanaopaswa kunufaika na mpango huo huenda ukafanyika hivi karibuni huku akisema kuwa serikali ina mpango wa kufanya usajili huo kila mwaka katika siku zijazo.

Amekariri kuwa wanaonufaika na fedha hizo watapokea fedha zao za mwezi februari kabla ya mwisho wa wiki hii.

Mpango wa Inua Jamii unahusu utoaji wa pesa kwa lengo la kusaidia walio katika mazingira magumu zaidi katika jamii

Subscribe to eNewsletter