Maeneobunge ya Laisamis na Moyale kaunti ya Marsabit yabainika kuwa na uwezo wa kuzalisha gundi na Resini.
July 10, 2025
Na Joseph Muchai
Wanaolengwa katika mpango wa kitaifa wa Inua Jamii watalazimika kusubiri kauli ya serikali ili kujua wakati wa kujisajili katika mpango huo.
Akizungumza na Shajara ya Radio Jangwani kwa njia simu mratibu wa huduma za umma katika kaunti ya Marsabit Vincent Musee Ndindi amesema kuwa kwa sasa serikilai kuu haijatangaza wakati zoezo la usajili litaandaliwa.
Muse ametoa wito kwa wanaohitaji kusajiliwa katika mpango huo kuwa na subira na kwamba serekali iwaweka wazi mipango yote kuhusu zoezi la kuwasajili watu.
Anasema kuwa mpango huo ni salama kwani hakuna nafasi ya madalali.
Inua jamii ni mpango wa serikali wa kusaidia wasio na uwezo katika jamii kujikimu kama anavyoelezea bwana Musee.
Mara ya mwisho watu kusajiliwa katika mpango huo ilikuwa mwishoni mwa mwaka jana.