KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Na Carol Waforo
Wito wa amani unaendelea kutolewa kwa wakaazi wa Marsabit na haswa walio katika maeneo ya mpaka wa kenya na Ethiopia.
Haya ni baada ya kushuhudiwa kwa visa vya utovu wa usalama katika eneo la Dukana nchini Kenya na eneo la Dillo nchini Ethiopia ambapo kijana moja raia wa Kenya aliuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Dukana huku nao watu watatu raia wa Ethiopia wakiuuawa nchini humo na wanne wakijeruhiwa ikiaminika ni kisa cha kulipiza kisasi.
Wito huu ulitolewa hapo jana wakati wa mkutano wa amani uliandaliwa katika kituo cha pamoja cha huduma cha mpaka wa Kenya na Ethiopia, upande wa taifa hilo jirani na kuwaleta pamoja washkadau katika idara ya usalama kutoka mataifa yote mawili, kamati ya amani jimboni Marsabit, serikali ya kaunti ya Marsabit pamoja na wazee wa vijiji kutoka Marsabit na wale wa nchi jirani ya Ethiopia.
Katika mkutano huo wazee wa jamii kutoka eneo la Dukana walitakiwa kufanya uchunguzi na kuhakikisha kuwa wahalifu waliotekeleza mauaji Dillo nchini Ethiopia wanakamatwa baada ya wale wa Ethiopia kusema kuwa tayari wahalifu watatu wanaodaiwa kutekeleza mauaji ya kijana huyo moja kule Dukana wamekamatwa.
Wazee hao sasa wanasema kuwa watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa hilo limefanyika.
Naibu mwenyekiti wa kamati ya amani Marsabit Adan Chukulisa anasema kuwa jamii kutoka pande zote mbili zimekubaliana kudumisha amani katika maeneo hayo ya mpakani.
Vilevile Chukulisa amezitaka jamii zote jimboni Marsabit kukumbatia amani iliyopo.
Mwanaharakati Hassan Mulata ambaye pia ni mwanachama wa kamati ya amani Jimboni Marsabit anasema kuwa jamii zote zimeonyesha nia njema ya kuhakikisha amani inarejea katika maeneo ya Dukana na Dillo.
Akiwakilisha wanawake katika mkutano huo mwasisi wa shirika la MWADO Nuria Gollo ametahadharisha jamii dhidi ya visa ya kulipiza kisasi.
Kamishana wa kaunti ya Marsabit James Kamau amesema kuwa mkutano sawia na huo utaandaliwa wiki ijayo ambapo jamii kutoka maeneo ya Dukana nchini Kenya na wale wa Dillo nchini Ethiopia watakuja na mkataba wa maelewano wa kudumisha amani katika maeneo hayo ambao pia utaangazia mikakati ya kushughulikia maswala ibuka.
Maeneo mengine Jimboni Marsabit yatajumuishwa katika mazungumzo hayo pamoja na baadhi ya wilaya kutoka taifa la Ethiopia.