KOSH UNITED KUTOKA KITURUNI NDIO MABINGWA WA TAJI LA NAPO CONSERVATIONS CUP MWAKA WA 2025.
April 25, 2025
Wananchi watakiwa kutoa taarifa ili kufanikisha operesheni ‘Ondoa Jangili’ Marsabit.
Na Mwanahabari Wetu
Huku operesheni Ondoa Jangili Marsabit ikiendelea wananchi wametakiwa kutoa taarifa muhimu ambazo zinaweza saidia katika kufanikisha operesheni hiyo.
Haya yalibainika hapo jana wakati wa mkutano wa amani kati ya taifa la Kenya na lile la Ethiopia kufuatia utovu wa usalama mpakani katika maeeneo ya Dukana na Dillo.
Akizungumza katika mkutano huo kamanda wa maafisa wa Jeshi la Ulinzi KDF walio katika kaunti ya Marsabit Luteni Kanali David Waigwa amesema kuwa operesheni hiyo inaendelea na itafanikishwa kwa ushirikiano wa jamii na serikali ambapo jamii imeombwa kutoa taarifa kwa idara za usalama.
Operesheni Ondoa Jangili ilizunduliwa na Huduma ya Kitaifa ya Polisi tarehe 3 Februari 2025, katika kaunti za Marsabit na Isiolo ikilenga kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usalama unaohusishwa na kundi la OLF linaloaminika kuendeleza uhalifu wa aina mbalimbali kupitia mpaka wa Kenya na Ethiopia.
Mapema mwezi huu Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu ya Kenya (KNCHR) ilikosoa ukiukwaji wa haki za binadamu unaodaiwa kutekelezwa na maafisa wa polisi wakati wa operesheni hiyo.
KNCHR ilieleza wasiwasi kuhusu ripoti za mauaji, utekaji nyara, na unyanyasaji wa raia na maafisa wa usalama.